Mapendekezo ya Bajeti ya Taifa

Taaluma ya Uhasibu ni miongoni mwa wadau ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakitoa mapendekezo ya awali ya bajeti kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)

Lengo kuu la mapendekezo ya awali ya bajeti ni kutoa muhtasari wa maeneo ya kuboreshwa yanayoweza kuzingatiwa na Serikali katika matayarisho ya bajeti ijayo ya Taifa kwa madhumuni ya kuongeza mapato/maduhuli ya Serikali, kukuza uchumi wa viwanda na kuboresha viwango vya maisha vya raia wake.

Wadau wa taaluma ya uhasibu kwa kawaida hualikwa kuwasilisha mapendekezo yao yaliyojumuishwa na kuwasilishwa na NBAA kwa Wizara yenye dhamana ya Fedha kwa majadiliano zaidi. Mapendekezo yaliyowasilishwa yanatakiwa kuwa na sababu za kina, kuweka ulinganifu na nchi nyingine, kama zipo, na mapendekezo ya kueleweka kwa urahisi na kuzingatiwa wakati wa majadiliano.