Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Je nikiwa sina masomo matatu niliyofaulu vizuri (credit) katika elimu ya Sekondari, lakini napenda kujiunga katika fani ya uhasibu, nifanye nini?

Kuna vyeti vingine vinavyotambuliwa na NBAA : kama cheti cha NABE hatua ya II na kufaulu masomo yasiyopungua manne uliyofaulu vizuri (passes grade) pamoja na cheti cha kidato cha nne(IV).

AU Barua ya Matokeo ya Hatua ya Msingi ikionyesha kuwa umefaulu mtihani huo ambao unaendeshwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.Zaidi ya hayo ni lazima uwe umemaliza elimu ya Sekondari ikionyesha masomo uliyofanya na kufaulu.

Masharti ya kujiunga kufanya mitihani ya ATEC I ni yapi?

Masharti ya kujiunga katika mitihani ya ATEC ni kuwa na cheti cha kumaliza elimu ya Sekondari na kufaulu vizuri (credit) masomo yasiyopungua matatu (3) na kufaulu (pass grade) masomo mawili (2) ikiwemo Kiingereza na Hisabati.

AU cheti cha kumaliza elimu ya sekondari kidato cha sita (VI) na kufaulu masomo makuu mawili au moja na somo la ziada, alimradi uwe umefaulu Hisabati katika Elimu ya Sekondari ya Kidato cha nne (IV) angalau kwa alama ya D.

AU Cheti cha mwaka mmoja kutoka chuo kinachotambulika pamoja na ufaulu wa alama ya D au zaidi katika masomo ya Kiingereza na Hisabati katika cheti cha kidato cha nne

AU Vyeti vingine ambavyo vitakavyoendelea kutambuliwa na Bodi wakati kwa wakati.

Ni mitihani gani inayoendeshwa na NBAA?

NBAA inaendesha mitihani katika ngazi mbili za kitaaluma; Mitihani kwa ajili ya Cheti cha Uandishi na Utunzaji Vitabu vya Hesabu Ngazi ya I & II (Accounting Technician Examinations – ATEC Level I & II) yenye masomo manne manne kila ngazi na Mitihani ya Kitaaluma ya Uhasibu – Professional Examinations ambapo mhitimu hupata shahada ya Uhasibu yaani Certified Public Accountant (CPA).Mitihani ya ATEC iko katika ngazi mbili ; ATEC 1 na ATEC II.Mitihani ya CPA iko katika hatua tatu ; Ngazi ya Msingi yenye masomo matano, Ngazi ya Kati yenye masomo sita na Ngazi ya Mwisho yenye masomo manne.

Nimemaliza elimu ya sekondari hivi karibuni. Je, ni kozi zipi ninazoweza kuchukua?

NBAA ni Taasisi ya kutahini na huwa hakiendeshi kozi zozote za uhasibu bali hushirikiana na vyuo vinavyoendesha masomo ya uhasibu ambavyo inavitambua ili viendeshe mafunzo hayo kwa wanafunzi wanaojiandaa kwa mitihani ya Bodi.