MWALIKO WA KUTOA MAONI KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA USAJILI WA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU

Imewekwa: Aug 10, 2021


Wadau wa Sheria ya Uhasibu na Ukaguzi nchini, mnakaribishwa kutoa maoni yenu kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) juu ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Usajili wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu uliosomwa mara ya kwanza tarehe 12 Februari, 2021.

Hivyo basi Wanachama na Vyama vya Kihasibu vilivyo chini ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu mnaombwa kuwasilisha maoni yenu kupitia anuani za barua pepe zifuatazo: cna@bunge.go.tz au kamati@bunge.go.tz na majadiliano yatafanyika katika kikao kitakachofanyikatarehe 12 Agosti 2021 katika kumbi za Ofisi ya Bunge ambacho kitapokea ana kwa ana maoni ya wadau wa Sheria tajwa hapo juu.

Nakala tete ya Muswada huu inapatikana kupitia Tovuti ya Bunge ambayo ni: www.bunge.go.tz.

Tunashukuru kwa ushirikiano

MKURUGEZI MTENDAJI

BODI YA TAIFA YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU (NBAA) 4 BARABARA YA UKAGUZI, “AUDIT HOUSE”, GHOROFA YA NANE, S.L.P. 1271, 41104 TAMBUKARELI, DODOMA, TANZANIA

Barua pepe: info@nbaa.go.tz Tovuti: www.nbaa.go.tz