MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI YA UMMA TAREHE 16-23 JUNI 2022

Imewekwa: Jun 16, 2022


Katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma, Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) inafurahi kuwatangazia wateja na wadau wake wote wenye maoni au changamoto kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Taaluma ya Uhasibu hapa nchini, ikiwemo: uanachama, elimu na mafunzo,utumiaji wa viwango vya hesabu vya kimataifa n.k kufika katika ofisi za Bodi zilizopo Jengo la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Dodoma, ghorofa ya nane, au jengo la Mhasibu, mtaa wa Bibi Titi Mohamed- Dar es salaam kuanzia tarehe 18 mpaka 23 Juni 2022 kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni

Pia unaweza kutuma maoni, malalamiko au ushauri kupitia baruapepe au anuani hapo chini.

WOTE MNAKARIBISHWA

Tafadhali wasiliana nasi kwa anwani ifuatayo:

Mkurugenzi Mtendaji

NBAA,

S.L.P 1271, DODOMA.

Simu na. +255-22-2211890-9

Barua pepe: info@nbaa.go.tz

Tovuti: www.nbaa.go.tz

IMETOLEWA NA CPA. PIUS A. MANENO

MKURUGENZI MTENDAJI

NBAA.